Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Safari ya Hawa wa Diamond yaiva, Babu Tale aivalia njuga

20654 Diamond+pic TanzaniaWeb

Thu, 4 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Siku chache baada ya msanii Diamond kuingilia kati matibabu ya msanii mwenzake Hawa Said ’Hawa Nitarejea’, inaelezwa kinachosubiriwa ni viza ya kumwezesha kuingia nchini India.

Mlezi wa Hawa anayesimamia matibabu yake, Pili Misanah, ameiambia MCL Digital kuwa tayari uongozi wa WCB kupitia meneja wake, Babu Tale wanashughulikia suala hilo.

“Hiyo viza itatupa mwanga ni lini hasa Hawa atasafiri, kwa kuwa nchi za watu huwezi kwenda kama unaenda Karikoo, nao wana taratibu zao ikiwemo kujua kama tuna uwezo wa kulipia matibabu hayo.

“Nashukuru pamoja na kwamba nipo namuuguza mwanangu, Babu Tale amekuwa akinisaidia kulishughulikia suala la Hawa na ninaamini hadi kufika kesho huenda ikapatikana,” amesema.

Hawa Said maarufu kwa jina la ‘Hawa Nitarejea’ anasumbuliwa na ugonjwa wa kujaa maji tumboni inayoelezwa kuwa inatokana na kuwa na tatizo la ini.

Kutokana na ugonjwa huo ameshalazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zaidi ya mara nne na kutolewa maji tumboni.

Septemba 29 mwaka huu, msanii Diamond kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter , Diamond alianika wazi kuwa ameamua kumsaidia ili aweze kupata matibabu zaidi na kueleza kuwa yatagharimu wastani wa Sh50 milioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz