Msanii mkongwe wa muziki wa taarabu Sabaha Salum amedai kuwa watoto wake wana sauti nzuri ya kuimba lakini hawapo tayari na wanaomba Mungu aache kuimba taarabu.
Akizungumza na waandishi wa habari mkongwe huyo wa muziki wa mwambao ameeleza kuwa watoto wake wanaomba aache kufanya muziki, japo na wao wana sauti za kuimba ila hawako tayari kujihusisha na masuala ya muziki.
Haata hivyo, msanii huyo ametoa wito kwa wanaotaka kufanya muziki wa taarabu kuwa wasiwe na wasiwasi muhimu ni kujitambua katika unachokifanya.
Msanii huyo ana takriban miaka 14 ndani ya muziki huo, amewahi kufanya nyimbo mbalimbali kama 'Niache nijivune', 'Hisani yangu', 'Tunapendana', 'Sihadhiriki', 'Aso mtu ana Mungu'.