Dar es Salaam. Mwigizaji wa filamu wa kike Wema Sepetu ametupwa gereza la Segerea kwa siku saba, baada ya kujisalimisha kutokana na amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliyotolewa akamatwe Juni 11.
Wema alijisalimisha jana na kukamatwa ikiwa ni siku sita baada ya mahakama hiyo kutoa amri na hati ya kumkamata kwa kushinda kufika kwenye kesi yake inayomkabili mahakamani hapo.
Mrembo huyo alipandishwa katika gari la Magereza jana mchana na kupelekwa mahabusu hadi Juni 24 Mahakama itakapotoa uamuzi wa ama kumfutia dhamana au la.
Awali, wakili wa Serikali, Gloria Mwenda alieleza Mahakama kuwa licha ya suala la ugonjwa kuwa sababu ya kibinadamu, alipaswa kutoa taarifa kupitia kwa wadhamini wake badala ya wakili wake.
Hivyo aliiomba mahakama itoe onyo kali dhidi yake kutoka na kosa hilo.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Kasonde aliamuru msanii huyo apelekwe mahabusu hadi Juni 24, atakapotoa uamuzi wa ama kumfutia dhamana au la.
Pia Soma
- Serikali ya Tanzania kumaliza kesi kwa mashauriano
- Dk Kigwagalla aanza kuhamasisha watu maarufu kupanda Mlima Kilimanjaroo
- Kesi ya Zitto yakwama kuendelea mahakamani