Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Sababu za wapenzi wengi kuchepuka

Mke Mume Couplees Sababu za wapenzi wengi kuchepuka

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mpenzi msomaji wangu, kasi ya kusalitiana kwa wapenzi imekuwa ikiongezeka kila kukicha kiasi kwamba unapoingia katika uhusiano wa kimapenzi unahisi kama unaingia kwenye matatizo makubwa na hii ni kwa sababu watu siyo waaminifu kabisa kwa wapenzi wao. Unaweza kuwa na mpenzi wako ambaye kila mnapoonana anakueleza kuwa, hawezi kukusaliti na atakuwa na wewe katika shida na raha.

Lakini huyohuyo usishangae siku moja ukamkuta yuko na mtu mwingine. Swali la kujiuliza ni kwamba, kwa nini wapenzi wanachepuka? Hicho ndicho nilichopanga kukizungumzia leo. Yaani nitaainisha baadhi ya mambo ambayo kwa uchunguzi wangu nimebaini ndiyo yanayochangia walio wengi kuchepuka, wawe wako kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida.

TAMAA ZA KIMWILI NA PESA Tamaa hasa ya pesa imekuwa ikiwashawishi watu kushindwa kujizuia kuwasaliti wapenzi wao. Kwa wale ambao wako kwenye ndoa wakati mwingine hasa wanawake wasipopatiwa mahitaji yao muhimu na akatokea jamaa na kumhakikishia kwamba atampatia kila anachotaka, wanakubali mara moja bila kujua kwamba wao ni wake za watu ama wapenzi wa watu na kujikuta wanajenga mazoea. Wengine wanapatiwa kila kitu na waume zao lakini sasa kinachotokea ni tamaa za kimwili tu ambazo zinawasumbua na kujikuta wanatafuta wanaume wengine huku wakidai kuwa wanatafuta ladha tofauti. Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia, unaweza kumkuta ana mwanamke bomba tu mwenye kila kigezo, lakini bado anakuwa na tamaa za kutafuta kimwana mwingine nje.

TABIA ZISIZORIDHISHA Wapo ambao wanaishi maisha ya ajabu sana, yaani wanaishi katika ndoa ama ndani ya uhusiano wakielekea kwenye kuoana lakini hawaaminiani kabisa, kila mtu anakuwa na wasiwasi juu ya mwenzake. Afadhali sasa iwe kutokuaminiana tu lakini wapenzi wanakuwa hawasalitiani. Kuna wale ambao ni wazi hawatulii katika mahusiano yao, yaani matendo yao tu yanaonesha dhahiri kwamba, uaminifu ni sifuri.

KUWEPO KWA MAPENZI YA KILAGHAI Tunapozungumzia mapenzi tunaweza kuyagawanya katika makundi mawili, mapenzi ya kweli na mapenzi ya uongo. Walio katika mapenzi ya kweli huwezi kuwasikia wamesalitiana. Ila wale walio katika mapenzi ya kudanganyana kusalitiana ni kitu cha kawaida kwao hivyo kujikuta kila siku wakifumaniana.

UDHAIFU KWA WAPENZI Udhaifu ambao umezungumziwa hapa ni wa kimaumbile ambao hata hivyo wataalam wa masuala ya mapenzi wanaeleza kwamba, haiwezi kuchukuliwa kama sababu ya kumsaliti mpenzi wako uliyempenda kwa dhati.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live