Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu wachekeshaji kuitwa ‘Chale’

Chale+pic Sababu wachekeshaji kuitwa ‘Chale’

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By SALIM SAID SALIM KATIKA jamii nyingi za Waswahili na hasa Zanzibar anapotokea mtu analifanyia mzaha jambo muhimu utasikia anaambiwa acha kufanya uchale yaani mzaha. Asili ya neno chale ni jina la mchekeshaji maarufu wa michezo ya sinema wa Kiingereza, Charlie Chaplin. Tangu siku alizopata umaarufu kwa mambo ya kuchekesha Waswahili wakabuni neno chale kumueleza mtu ambaye anafanya vichekesho.

Katika nchi nyingi siku hizi watu hufanya sherehe za kukumbuka visa na mikasa ya mtu huyu pale inapowadia siku aliyozaliwa.

Bwana huyu, Charles Spencer “Charlie” Chaplin alizaliwa 1889 na kufariki duni 1977.

Kwa zaidi ya miaka 75 alishiriki katika michezo zaidi ya 50 ya sinema tangu mdogo hadi ali-pokuwa mzee na kuvutia wakubwa na wadogo duniani kote. Tokea wakati wa uhai wake na baada ya kuiaga dunia watu wamekuwa wakifurika kwenye majengo ya sinema kuangalia michezo yake. Wengine wengi wanazo majumbani mwao sahani za michezo yake. Vituo vya run-inga katika nchi nyingi havichukui muda mrefu bila ya kuonyesha mchezo wa Charlie Chaplin. Hata hapa kwetu ukipanda boti zinazosafiri kati ya Dar es Salaam na Zanzibar utaona michezo ya Charlie Chaplin inaonyeshwa.

Hii husababisha wakati wote wanaosafari kufurahi na kuwaacha hoi kwa vichekesho vya Chaplin tangu mwanzo hadi mwisho wa safari.

Charles Spencer “Charlie” alikuwa mcheza sinema mchekeshaji maarufu kuliko wenzake wote wa fani hiyo duniani.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz