Drama Queens au Big 6; ni lililokuwa kundi la mastaa kike wa Bongo Movies, Irene Uwoya, Kajala Masanja, Wema Sepetu, Jacqueline Wolper, Elizabeth Michael (Lulu) na Aunty Ezekiel ambao walipanga kufanya makubwa, lakini wamesambaratika.
Uchunguzi wa Gazeti la IJUMAA umebaini kwamba, kundi hilo lilipanga kufanya kipindi maalum (reality show) ya maisha yao ambapo kampuni mbalimbali zilianza kuwafuata kutaka kuchukua dili hilo.
Imeelezwa kuwa, kundi hilo halikudumu hata mwezi mmoja kwani walianza kupigana majungu ya chini kwa chini, kuigana na kunyang’anyana madili huku Wema akidai kutengwa kutokana na kutokuwa na mtoto ilihali wenzake wote wana watoto.
Imebainika kuwa, watu kama Wolper na Lulu walibanwa na majukumu ya kulea kwani walitoka kujifungua kisha kubeba ujauzito kwa mara nyingine.
Kwa upande wake, Uwoya aliendelea kuwa bize na mambo yake ya kula bata huku Aunty akiwa bize na majukumu yake na familia yake na msanii Kusah.
Kajala yeye alidaiwa kuwa bize na majukumu mapya ya kumsimamia mchumba’ke, Harmonize na kuachana na projekti hiyo ya Big 6.
Baada ya mambo kwenda mrama, ni rasmi sasa hakutakuwa tena reality show ya Big 6 na kampuni iliyotaka kusaini nao dili hilo la pesa nyingi nayo imeingia ubaridi kwa kuangushwa na mastaa hao.