Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saa ya Diamond Yazua Tafrani

Diamond Saa Mpya Diamond

Mon, 18 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ghafla mji umekuwa mzito! Miongoni mwa mijadala mikubwa kwenye uwanda wa burudani Bongo ni saa ya bei mbaya aliyonunua Diamond Platnumz nchini Marekani aina ya Rolex aliyodai ameinunua kwa shilingi milioni 69 za Kitanzania na kusema acheni kuvaa vitu feki mtapata kansa ya mkono.

Taarifa ikufikie kwamba, ishu hiyo imezua tafrani ya aina yake ambapo kila mtu anasema lake.

Baadhi ya watu wanasema bei aliyotaja Diamond si sahihi baada ya kuvuja kwa risiti aliyonunulia saa hiyo ikionesha amenunua Dola za Kimarekani 25,000 (sawa na shilingi milioni 57 za Kitanzania).

Hapa swali kuu ni kwamba Diamond amedanganya na kusema milioni 69 au risiti ndiyo imedanganya?

Kuhusu bei, Baba Levo anasema yeye anavyojua akiwa kama mtu wa karibu wa Diamond au msemaji wake wa kujitakia almaarufu Blue Chawa, saa hiyo imegharimu shilingi milioni 73.

Kwa upande wake, Dokta Kumbuka anasema kuwa, saa kama hiyo ni ghali kuliko baadhi ya magari ya baadhi ya mastaa Bongo, lakini yeye anaamini Diamond ana uwezo wa kununua saa hata ya shilingi milioni 800.

Mtu mwingine aliyeguswa na ishu hiyo ni Mwijaku ambaye anasema saa hiyo ni feki na inauzwa shilingi elfu nane huko Mburahati jijini Dar kwani orijino yake haiuzwi bei hiyo kwani amenunuliwa saa hiyo na mkewe kwa zaidi ya Dola 100,000 (zaidi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania!

Naye mmoja wa mashabiki kindakindaki wa Harmonize anasema Diamond ameona aanze kutumia vitu kama hivyo baada ya kuona hamuwezi tena Harmonize kimuziki.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Google, aina hiyo ya saa inagharimu Dola za Kimarekani 107,814 (laki moja na elfu saba, mia nane na kumi na nne) ambazo ni zaidi ya milioni 220 za Kitanzania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live