Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

STEVE NYERERE AWACHANA BILLNASS NA NANDY "MTAKUFA NA MISIFA YENU"

Image 765.png STEVE NYERERE AWACHANA BILLNASS NA NANDY "MTAKUFA NA MISIFA YENU"

Mon, 23 Nov 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Msanii wa filamu nchini Tanzania Steve Nyerere amewatolea povu wapenzi ambao ni Billnass na Nandy baada ya kuposti picha yao wakiwa barabarani wamelala huku wameweka poz la ku-kiss na kusema kitendo hicho kinahatarisha maisha yao.

“Mtakuja kufa misifa yenu hiyo haya, jifanyeni kama nyie ndiyo wa kwanza kupendana, watu wanajua mapenzi toka 1981 lakini hawajawahi kucheza na barabara, sisi tunataka kusikia shemeji kaingia leba, hayo mnayofanya hata sisi kwenye sinema tunafanyaga nyau nyie” ameandika Steve Nyerere 

Ukiachana na Steve pia wapo wasanii wengine waliendelea kukoment ikiwemo Idris sultani, Dj.Choka na Roma mkatoliki.

Mapenzi yenu yanaweza kuwa yamoto ila sio ya moto kama hiyo barabara ndugu zangu” Comment ya Idris Sultan

Kuna saa natamani ningekuwa mimi ndiyo hiyo lami” Dj Choka

Ooooh, mkijagongwa na gari hapo hasara kwa nani, halafu mbona kama Billnass hauna furaha kwani umelazimishwa kwenda” Roma Mkatoliki

Chanzo: zanzibar24.co.tz