Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SSK kuja na albamu mwaka huu

3940 16465409 412389589104498 5296151965430972416 N TZW

Mon, 5 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kundi la muziki wa hip hop Bongo, SSK wanatarajia kutoa albamu kwa mwaka huu.



Member wa kundi hilo Wakazi ameiambia Bongo5 kuwa baada ya albamu yake ‘Kisimani’ kutoka watatoa kazi za kundi kisha albamu.

“Baada ya albamu yangu ya Kisimani SSK project lazima itakuwa inafuata kwa sababu na sisi lazima tuachie albamu katikati ya mwaka ili tuweze kufanya tour kirahisi,” amesema.

Katika hatua nyingine Wakazi amezungumzia ukimya wa kundi hilo kwa kusema kila mmoja alikuwa na project zake binafsi.

“Tatizo ilikuwa albamu yangu na ZaiiD amekuwa buys na tour kwa sababu ngoma yake ‘Wowowo’ ilifanya vizuri, so alihusika tour za Fiesta sasa anafanya tour zake binafsi,”  amesema.

Chanzo: bongo5.com