Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

SARA WA HARMONIZE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU NDOA YAKE

Capture 534?fit=375%2C333 SARA WA HARMONIZE AFUNGUKA MAZITO KUHUSU NDOA YAKE

Sat, 5 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Kupitia ukurasa wa kijamii wa Instagram wa mke wa msanii Harmonize bibie Sarah ameandika ujumbe mzito kuhusuana na ndoa yake na msanii huyu .

“Niliolewa na wewe sababu nilikupenda, ulikuwa kila kitu kwangu na nilikuchagua kama ulivyokuwa na nikakupa mapenzi yangu yote na nilijitahidi kukupa furaha ambayo wewe hukuweza kunipatia.

Siku baada ya siku nimekuja kugundua kuwa upo tofauti kabisa na huna adabu kwa mtu yeyote. Na hukujua kumtunza mwanamke kama mimi au kujivunia kwa mtu ambaye amekupa maisha mazuri.

Na hujui kuheshimu watu waliokupenda na waliokuwa wanakusapoti. Muda mwingi nagundua kuwa wewe ni muongo na bandia kwa kila kitu.

Nimepitia mengi kwenye haya mahusiano x ndoa na kama nikiviweka vyote hapa kila mtu atashangaa sababu unasuka tofauti kabisa.

Siku zote unavaa kinyago usoni pako. Sina hata maneno mengi yakusema kwa sasa .. hujawahi kushukuru hata siku moja kwaniliyokufanyia na sasa umechelewa.

Maisha yatakufundisha somo ambalo unastahili kwa vitu vyote ulivyonifanyia na kwasasa nitazingatia maisha yangu “

Chanzo: zanzibar24.co.tz