Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SAKATA LA MWANA FA, AY NA TIGO LAMALIZIKA

Fa Pic Data?fit=445%2C344 SAKATA LA MWANA FA, AY NA TIGO LAMALIZIKA

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Hukumu iliyoamuru wanamuziki Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) na Ambwene Yesaya (AY), kulipwa Shilingi Bilioni 2.1 na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya kampuni hiyo kukiuka sheria za hatimiliki Mahakama Kuu imetengua hukumu hio.

Jaji Joacquine De-Mello amekubaliana na rufaa ya kampuni ya Tigo kuwa mahakama ya wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Tayari kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Tigo ilishawalipa Mwana FA na AY fedha hizo.

Mwezi Aprili mwaka 2016, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Ilala, alitoa amri ya Wanamuziki hao kulipwa kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya kampuni ya Tigo.

Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo amesema atawaandikia barua Wanamuzìki hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa.

Chanzo: zanzibar24.co.tz