Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

SAFARI YA MWISHO WA MZEE JENGUA, MAELFU YA WATU YAJITOKEZA

Capture 583?fit=741%2C420 SAFARI YA MWISHO WA MZEE JENGUA, MAELFU YA WATU YAJITOKEZA

Thu, 17 Dec 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Siku ya jana Disemba 16 ni siku ambayo itakumbukwa na wapenzi wa filamu nchini Tanzania baada ya msiba mkubwa wa aliyekuwa muigiza nguli Marehemu Mohd Fungafunga maarufu kama Jengua kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele.

Marehemu Mzee Jengua amefariki dunia siku ya Jumanne Disemba 15 nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga Mkoa wa Pwani baada ya kuugua.

Mamia ya watu waliojitokeza kumuaga katika safari yake ya mwisho na kwa ajili ya kwenda kuzika kwenye makaburi ya Mburahati Jijini Dar Es Salaam.

Pia wachekeshaji na mastaa wa filamu walijitokeza kwa wingi kumshindikiza mwenzao ikiwa ni ishara ya upendo na mshikamano mkubwa walio nao baadhi ya wasanii hao ni kama Steve Nyerere, Miss Lucy Charles, Mzee Jumbo, Kingwendu, JB, Mama Kanumba, Patrick Kanumba, Bi Staa, Tito, Ringo, Tin White, Kivurande na Hashim Kambi ni baadhi ya mastaa waliojitokeza

Chanzo: zanzibar24.co.tz