Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ryan Garcia: Namjua aliyemuua Tupac

Ryan Garcia Na Tupac. Ryan Garcia na Tupac.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa Marekani Ryan Garcia anasema kwamba anamjua aliyemuua Tupac. Kupitia "Twitter" X ameandika;

"Mtaniamini kama nikiwaambia ninamjua aliyemuua Tupac? Wengi wenu mnajua jibu.. Ila ninaweza kuwathibitishia," amesema Ryan Garcia.

Kumbuka mwaka jana sakata la kifo cha Tupac lilichukua sura mpya baada ya mshukiwa namba moja Keef D kukiri mbele ya polisi kwamba alihusika na mauaji ya Tupac lakini alitumwa na Rapa #Diddy kwa ahadi ya dola za Kimarekani milioni 1.

Tupac aliuawa kwa kupigwa risasi huko Las Vegas, mwaka 1996.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live