Unaambiwa stori ya Harmonize kuweka bango barabarani sio ishu, lakini ishu ni ujumbe aliouambatanisha kwenye picha yake katika bango hilo, unaosomeka "Single Again" baada ya kuachana na Kajala.
Sasa mashabiki wameachwa na maswali kedekede iwapo Mmakonde huyo anataka kuja na ngoma mpya hivyo anatengeneza tension kwa vyombo vya habari na mashabiki ama kuna kitu kingine zaidi ya hicho.
Hata hivyo, mrembo aliyewahi kuwa mke wa Msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara, Rushaynah amehoji kwamba mkali hiyo kufuatia ujumbe wake huo katika bango "Anajiuza..!"
Wawili hao ambao wanatajwa kuwa ni marafiki, kwani Rushaynah alishawahi kuonekana nyumbani kwa Konde, Mbezi Beach siku chache tu baada ya kuachana na mumewe huyo wa ndoa.