Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rukia: Nilipishana na Mbosso

Mbosso Rcuky.jpeg Rukia: Nilipishana na Mbosso

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mrembo @rukiarucky ambaye ni mzazi mwenza wa @mbosso_ ameamua kuvunja ukimya na kufunguka sababu iliyopelekea wawili hao kutoishi pamoja tena licha ya kuwa kwenye uhusiano kwa miaka mingi.

Akipiga stori na Refresh ya Wasafi TV, Rukia amesema; “Mimi na Mbosso tulipishana kidogo, wakati nikiwa na mimba, ilikuwa kisirani cha mimba….! ‘Sitaki, toka wewe, nenda…’ kuanzia hapo hatukuwahi kukaa tena kuzungumza mambo ya kuishi pamoja.

“Muda wote Mbosso yupo nyumbani kwangu ila kwake siendi na sijawahi kwenda kwa sababu kwanza sipajui. Lakini kama muda wote yupo nyumbani kwangu kuna haja gani ya mimi kwenda kwake, kule namfuata nani?

“Sisi ni watoto wa Kiislam, kwa hiyo kuishi na mwanaume mpaka akuoe. Nitashukuru kama Mungu akijalia nikaolewa na Mbosso,” amesema Rukia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live