Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruge azitawala ‘status’ za mtandao wa WhatsApp

43992 Pic+ruge Ruge azitawala ‘status’ za mtandao wa WhatsApp

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kizuri hakidumu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Watanzania wengi kuonyesha kuumizwa na kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba.

Baada ya taarifa kutangazwa kupitia leo Jumanne Februari 26,2019 kupitia televisheni na mitandao mbalimbali ya kijamii, Watanzania wametumia simu zao za mkononi na kurasa zao za mitandao ya kijamii kuhani msiba huo mzito.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wengi wamejikuta wakiweka picha na jumbe za simanzi kuhusu kinara huyo wa tasnia ya burudani nchini katika mitandao ya kijamii ikiwemo ‘status’ za mtandao wa WhatsApp.

“Hakika duniani tunapita, milima ndiyo itabaki milele,” ni kati ya maneno ambayo yameandikwa na walio wengi kwenye status zao.

Pamoja na kutawala ‘status’ pia, mitandaoni ya kijamii kama facebook, Instagram na Twitter watu mbalimbali wamezungumzia msiba huo.

Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameandika kwenye Twitter yake, “Sisi sote ni wa Mungu na kwake tutarejea. Ruge umelala moja kwa moja lakini maisha yako ni mafunzo kwetu tuliobaki.”

Mchora vibonzo maarufu, Masoud Kipanya yeye ameandika, “Hakika sisi sote ni wa kwake na kwake tutarejea.”

Soma zaidi: Kusaga kutoa ratiba ya mazishi ya Ruge



Chanzo: mwananchi.co.tz