Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruge Mutahaba alivyopambana miezi nane kuokoa maisha yake

43977 Pic+ruge+3 Ruge Mutahaba alivyopambana miezi nane kuokoa maisha yake

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Amepigana kiume. Ndivyo unavyoweza kusema juu ya Ruge Mutahaba ambaye alipambania uhai wake kwa miezi nane katika hospitali mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Mwanzoni mwa mwaka jana, tarehe kama ya leo alikuwa mzima wa afya akiendelea na majukumu yake akiwa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group.

Soma zaidi: Gharama za matibabu ya Ruge zafikia Sh650 milioni

Katikati ya mwaka jana ndipo afya yake alipoanza kutetereka na Juni 2018 alikwenda mwenyewe nchini India kwaajili ya matibabu.

Katika moja ya makundi ya WhatsApp, aliaga kuwa anakwenda kufanya uchunguzi wa afya yake na angerejea wiki tatu baadaye.

Ingawa alichelewa kurudi tofauti na alivyotazamia, lakini alirejea na Agosti 21,2018 alionekana katika msiba wa Monica Magufuli ambaye ni dada wa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Ruge alikuwa miongoni mwa waombolezeaji walioshiriki mazishi ya Monica yaliyofanyika Chato mkoani Geita.

Baada ya hapo hakuonekana na taarifa zilisema alizidiwa na kulazwa katika hospitali ya Kairuki, jijini Dar es Salaam.

Oktoba mwaka 2018 alipelekwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu zaidi ambako alikaa mpaka alipofikwa na umauti leo Februari 26,2019.

Soma zaidi: Ruge Mutahaba afariki dunia, Rais Magufuli amlilia

Ruge aliyezaliwa mwaka 1970 katika Mji wa Brooklyn, New York nchini Marekani. Apata elimu ya msingi Shule ya Arusha darasa la kwanza hadi la sita kisha akahamishiwa Shule ya Mlimani jijini Dar es Salaam alipohitimu darasa la saba.

Baada ya kuhitimu, alijiunga na masomo ya kidato cha kwanza hadi cha nne shule ya sekondari Forodhani na baadaye Pugu Sekondari kwa masoko ya kidato cha tano na sita.

Soma zaidi: Zamaradi anavyomzungumzia Ruge, michango ya matibabu

Hakuishia hapo, Ruge aliendelea na masomo katika Chuo Kikuu cha San Jose cha California alipohitimu shahada ya masoko na baadaye akasoma shahada fedha katika chuo hichohicho.

Soma zaidi: Nape, Mwigulu, Sugu wamlilia Ruge

Endelea kufuatilia Mwananchi kupata taarifa zaidi



Chanzo: mwananchi.co.tz