Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruby hana mpango wa kuolewa tena baada ya kumpoteza Kusah

KUSSAH RUBY AUNT Ruby hana mpango wa kuolewa tena baada ya kumpoteza Kusah

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa mara nyingine msanii wa Bongo Fleva, Ruby amesisitiza hana mpango wa kurudi kwenye ndoa tena, miaka michache baada ya kuachwa na babydady wake Kusah ambaye alipata penzi jipya kwa muigizaji Aunty Ezekiel.

Kupitia Instastory yake, Ruby alipakia klipu ya mchungaji Rose Shaboka akihubiri kuhusu wanawake wanaojihisi kutokamilika bila ndoa.

Kwenye klipu hiyo, Ruby aliweka wazi kwamba hawezi tena kuwa kwenye kundi la warembo wanaohisi kutokamilika bila ndoa, akisema kuwa yeye na ndoa basi.

“Msichana anaona kama sijaolewa I am not complete. Kama sina mwanamume maisha yangu hayajakamilika, who said so? Katika kifungu kipi au Biblia gani?” Mchungaji huyo alihubiri.

Ruby akaipakia na kuongeza maandishi akisema;

“Ndoa my foot. Sitaki matatizo mimi yangu yamenitosha.”

Kusah na Ruby walikuwa wapenzi ambapo pia walibarikiwa kuwa na mtoto mmoja na Kusah katika mahojiano kadhaa amekuwa akinukuliwa akisema kwamba Ruby alimfungia hawezi kumuona mwanawe hata kidogo.

Alipoulizwa ni kwa nini hataki kumruhusu Kusah kumuona mtoto wao, Ruby alimsuta Kusah vikali kwa kusema kwamba msanii huyo hana lolote hata hela ya kuunga bando kwenye simu yake ni mtihani mkubwa, sembuse kumhudumia mtoto!

Mrembo huyo pia aliendeleza kumtuhumu msanii huyo katika mahojiano mengine kuwa wakati wapo pamoja, alikuwa anampeleka kwa waganga wa dunia.

Kwa upande wake, Kusah alikuwa akionekana sana na muigizaji aliyemshinda umri mara dufu, Aunty Ezekiel katika njia za ukakasi kiasi kwamba wengi waliamini wawili hao wapo katika mapenzi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live