MWANAMAMA mkali kunako anga la muziki mtamu wa Bongo Fleva, Hellen George Majeshi amefunguka ukaribu wake na mmoja wa mameneja wa Diamond Platnumz ambaye ni Babu Tale.
Hii ni baada ya maneno kusambaa kuhusiana na Babu Tale kumsaidia Ruby pesa za matumizi ya mtoto aliyezaa na msanii Kusah ambaye ametimkia kwa Aunt Ezekiel.
Ruby anasema kuwa, Babu Tale ndiye mtu ambaye alimfanyia koneksheni ya kwenda Coke Studio miaka kadhaa iliyopita hivyo ni kama kaka yake.
“Babu Tale ni kama kaka’ngu na ndiye mtu ambaye alinifanyia mimi mpango mpaka nikaenda Coke Studio na nilishawahi kufanya nao kazi kipindi kile cha Yamoto Band, kama amenisema kinyume, mimi najisikia faraja sana kwa sababu mimi kwa upande wangu naangalia ile baraka ambayo niliipata kutoka kwake, hayo mambo mengine ya mtu kutokujisikia vizuri, mimi hayanihusu,” anasema Ruby.