Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ruby Adai Kilichomkera Kwenye Mahusiano yake na Kusah ni Uchawi

Ruby Kusah Ruby Adai Kilichomkera Kwenye Mahusiano yake na Kusah ni Uchawi

Thu, 27 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

HATIMAYE mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Hellen George 'Ruby' amejibu kuhusu jambo ambalo liliwahi kumkera kwenye mahusiano yake na mzazi mwenzake, Kusah ambaye kwa sasa ni mpenzi wa Aunt Ezekile na tayari wana mtoto.

Ruby kupitia Insta story yake akijibu moja ya maswali ya mashabiki zake amesema kuwa jambo lililomkera kuhusu Kusah ni suala la uchawi (imani za kishirikina) kutoka kwa aliyekua mpenzi wake huyo ambae amefanikiwa kuzaa nae mtoto mmoja wa kike.

Hata hivyo Ruby hakufafanua zaidi kuhusu madai hayo, zaidi ya kujibu tu kwa ufupi katika kile alichodai kuwa anajiskia kuwa mkweli.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live