Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rubani anusurika kifo sekunde chache kabla ya ajali

Hux Rubani anusurika kifo sekunde chache kabla ya ajali

Thu, 23 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ni kunusurika kwa aina, kwamba muda mfupi baada ya tukio hilo Novemba mwaka juzi, rubani anayejulikana kama Hux anasema alikuwa na sekunde chache tu ya kujinusuru.

Uchunguzi rasmi ulihitimisha kupotea kwa nguvu kwa ghafla wakati wa kupaa kwa ndege hiyo pengine kulisababishwa na kifuniko kilichoachwa wazi kwenye moja ya sehemu za ndani za ndege.

Simulizi kamili ambayo sasa inapatikana kwenye filamu, inaeleza namna ndege hiyo ilipopoteza nguvu ghafla na rubani anasimulia:

"Nilijaribu kutafuta nguvu za dharura hiyo haikufanya kazi, kisha nikajaribu kupiga breki hiyo pia haikufanya kazi, kwa hiyo, nilijua kuwa itatoka nje ya meli."

Maisha ya Hux yaliokolewa na kifaa cha kiti chake  kiitwacho ‘ejector’ ambacho anakielezea kuwa cha teknolojia ya juu zaidi duniani. Sasa anaitaja hiyo ni bahati aliyokuwa nayo.

Parachuti yake alipoiwasha, anasema aliiona bahari chini yake na kisha sekunde moja baadaye akaona eneo la chini la meli likianza kuonekana kadri anavyoshuka, akihesabu nayo ni hatari nyingine.

Rubani huyo akafanikiwa kufika kwenye meli umbali wa wa futi chache, kabla ya kuvutwa tena na parachuti hadi mahali salama. Anaeleza, iwapo angetua kwenye meli hiyo, angeingia katika hatari ya kuburutwa chini ya meli hiyo ya kivita.

Uchunguzi rasmi ulihitimisha kuwa kupotea kwa ghafla kwa nguvu za umeme katika ndege hiyo labda kulisababishwa na kizuizi kifuniko kilichoachwa wazi kimakosa ndani ya ndege.

Ni ndege ambayo ni ya kisasa zaidi duniani, inayoendeshwa kwa pamoja nchini Uingereza na Jeshi la Wanamaji. Baadaye ilipatikana chini ya bahari.

Chris Terrill, ambaye alirekodi filamu hiyo, anasema ajali hiyo ya F-35 "ilikuwa mshtuko kwa kila mtu", lakini akasema majibu ya kampuni ya meli yalikuwa"ya haraka kwani ilikuwa tukio la kushangaza".

"Ndege pengine ingepotea, lakini kulikuwa na rubani, mwenza ambaye alipaswa kuokolewa," anafafanua.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live