Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rotimi: Afrika ni matajiri kuliko Marekani

Rotimi One Two.jpeg Rotimi

Mon, 1 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muigizaji na msanii wa muziki ambaye pia ni shemela wa taifa, Olurotimi Akinosho "Rotimi" amesema kuwa Afrika ni matajiri kuliko hata Marekani na kwamba ni kheri kuishi Africa.

Muimbaji huyo aliyetamba sana na nyimbo ya 'Love Somebody' alisema kuwa, "Watu wengi hawajui tu! Rudini Africa mkatembee, Afrika ni tajiri sana. Marekani kuna utajiri ila Afrika kuna matajiri,"

Rotimi ambae yupo katika penzi zito na msanii kutoka nchini Tanzania, Vanessa Mdee, aliendelea kusisitiza kuwa, "Ukiwa una hela Africa, haijalishi nchi gani, utaishia vizuri mara 10 zaidi kuliko watu wengi matajiri Marekani."

"Kila kitu cha Marekani kimeibiwa kutoka Africa," alisema Rotimi na kuongeza kuwa; "Marekani unapumuwa matatizo tu, kule hata hali ya hewa ni nzuri."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live