Rosa Ree mwanamuziki wa hip hop ambaye alichumbiwa aibuka kumpinga Rosa Ndauka ambaye pia ni rapa aliye katika ndoa.
"Ewe binti ukishajiona umefikisha miaka 27 achana na mambo ya kutafuta boyfriend tafuta mume, aje kujitambulisha kwenu akuvishe pete akuoe!!" aliandika Rose Ndauka.
Rosa Ree aliona ujumbe wa Rose na kumjibu kwa kuandika;
"Anaweza kuja akuvishe pete na bado akutende na akuache! Kutafuta mume isiwe focus, bora tutafute pesa tu, mambo mengine yanakuja kwa muda wake!" - amesema Rosa Ree.
Kwa upande wako wewe hapo unakubaliana zaidi na maoni ya nani kati ya warembo hao ambao mmoja ni mwanandoa na mwingine ni mwanamchumba?