Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rose Ndauka, Harmorapa kutangaza utalii mikoa ya Kusini

75985 Ndauka+pic

Tue, 17 Sep 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Msanii wa filamu nchini Tanzania,  Rose Ndauka na wa Bongofleva, Harmorapa ni kati ya wasanii watakaokuwa mabalozi katika kutangaza utalii wa mikoa ya Kusini.

Hayo yamebainika leo Jumatatu Septemba 16, 2019 katika mkutano kati ya balozi wa utalii nchini Tanzania,  Nangasu Warema na waandishi uliolenga kuzungumzia maonyesho ya utalii wa Kusini yatakayofanyika mkoani Lindi Septemba 20 hadi 22,2019.

Nangasu amesema Rose Ndauka, Harmorapa ambaye jina lake halisi ni Athumani Omar, Mkali Wenu na Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune ni miongoni mwa watu watakaofanya nao kazi katika kutangaza utalii wa Kusini.

"Watu wengi hawajui kama Kusini mwa Tanzania nako kuna vivutio vingi vya  utalii, naamini kupitia wasanii hawa tutashirikiana katika kuvitangaza na watu kwenda kutembelea," amesema.

Rose Ndauka amesema kupitia ubalozi aliopewa anaamini atayajua mengi  ya kuwafahamisha watu kuhusu utalii uliopo Kusini.

"Nasikia kuna kivutio kinaitwa Bustani ya Mungu kuna maua yanaota bila kumwagiliwa wala kuwekewa mbolea na vingine vingi ambavyo nikivijua vyema nitakuwa balozi mzuri  kwa watu wengine kuelezea uzuri wake," amesema.

Pia Soma

Advertisement
Pia, Harmorapa amesema akiwa mzaliwa wa Kusini ana kila sababu ya kujivunia utalii ulioko huko na kuongeza kuwa yeye ni shahidi wa uzuri wa vivutio hivyo.

Ameomba watu wasisite kwenda kuwekeza biashara mbalimbali.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz