Baadhi ya Wachungaji na waumini nchini Kenya wakiongozwa na Prophet Allan Jomba wamelalamika kwa kupaza sauti wakidai kwamba Mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania, Rose Muhando amekimbia na mamilioni ya pesa kutoka katika sehemu tofauti-tofauti nchini humo.
Akizungumza kwa masikitiko makubwa mbele ya waumini wake, Prophet Allan Jomba amesema waliandaa mkutano kanisani kwao na wakataka awepo Mwimbaji mmoja mkubwa ambaye ataunogesha mkutano huo, ambapo kwenye chaguzi zao walimchagua Rose Muhando atumbuize katika siku hiyo.
Baada ya kumchagua walimpigia simu wakamualika na yeye bila hiyana akasema atatokea siku ya Tamasha.
Prophet Jambo amesema Rose Muhando alitaja dau lake ambapo alisema lazima wamlipe laki mbili kwa pesa ya Kenya lakini pia pesa ya usafiri elfu 50 ya Kenya, ambapo walitekeleza majikumu yao kwa kumtumia pesa hizo zote.
Baada ya kutengeneza bango na kuliposti katika mitandao ya kijamii, Wachungaji wengine waliibuka wakidai kwamba hata kwao amechukua pesa na amewambia atakuwa na nafasi kwenye siku hiyohiyo ambayo alimuahidi Prophet Jambo.
Watu wanne kutoka sehemu mbalimbali walijitokeza na wao wakidai kwamba hata kwao Rose Muhando amechukua laki mbilimbili za Kenya na ameahidi atafika.
Hata hivyo baada ya siku ya tukio kufika, inadaiwa Rose Muhando alienda sehemu moja tu hizo sehemu nyingine hakwenda akidai kwamba anaumwa jipu kwa hivyo hataweza kufika sehemu ya tukio na ndio ukawa mwisho wa mawasiliano akatokomea na peza za waumini.
Hata hivyo, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rose Muhando amekanusha madai hayo ambapo amesema kama wanaomtuhumu wana ushahidi basi wampeleke Mahakamani.