Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rose Manfere ndiye Miss Tanzania

7d25ac61b8a13dd7ff96b24dbdc04b14 Rose Manfere ndiye Miss Tanzania

Mon, 7 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MREMBO Rose Manfere (katikati aliyeketi) ametwaa taji la Miss Tanzania, katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Dar es Salaam jana.

Rose aliwabwaga wenzake 19 kwa kuonesha mikogo tangu walipoanza kupita jukwaani na kuonesha vipaji tofauti na kufanikiwa kumrithi Queen Elizabeth Makune aliyemaliza muda wake.

Mshindi huyo aliingia katika tano bora na Juliana Rugumisa, Prisca Lyimo, Hoyce Bakanoba na Yvonne Paul katika Shindano hilo lililoandaliwa na kampuni ya The Look na mwaka huu lilikuwa na kauli mbiu ya ‘Urembo ni heshima.’

Warembo wengine walioshiriki ni Tamia Hakam, Rehema Cuthbert, Ruth Benitho, Grace Machibula, Margaret Mwambi, Sarafina Mageye, Martha Golodi, Zenitha Chundu na Deolyn Mollel.

Kwa ushindi huo Rose anayetarajiwa kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia mwakani yatakayofanyika nchini Brazil na alizawadiwa gari aina ya Subaru.

Katika mpambano huo mgeni rasmi alikuwa Naibu Spika Dk Tulia Ackson ambapo akizungumza mbele ya wageni waalikwa alimuomba muandaaji wa mashindano hayo, Basilla Mwanukuzi kuendeleza vipaji vya warembo wengine waliomfuatia Miss Tanzania huyo.

Kampuni ya Look inaandaa shindano hilo kwa mara ya tatu mfululizo tangu mwaka 2018 ilipochukua umiliki wa awali wa kampuni ya Lino International Agency baada ya kufungiwa.

Chanzo: habarileo.co.tz