Uongozi wa Rapa Rosa Ree umeweka wazi kuwa rapa huyo kwa sasa yupo na Familia yake akipatiwa Msaada baada ya kuleta sintofahamu katika Mitandao ya kijamii kwa kile alichokipost akisema kuna Magumu anayapitia.
“Tunatoa shukurani za dhati kwa upendo na ushirikiano mnaoendelea kumuonesha Rosa Ree kwa wakati huu. Yupo na familia yake kwa sasa na wanahakikisha anapata msaada anaohitaji. Tunaomba mumruhusu nafasi wakati huu wa mapito. Sala zenu na ushirikiano katika kumtia nguvu ni muhimu."
Rose Ree alitangaza jana asubuhi kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa hayupo sawa na anapita mambo magumu ambayo hakuyawa wazi.