Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rosa Ree amlipua Khaligraph Jones kwa verse

Khaligraph (5).jpeg Khaligraph Jones na Rosa Ree

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya rapa wa Kenya, Khaligraph Jones kuandika kupitia Instagram page yake akiwaponda wasanii wa Hip hop Bongo kwamba hawawezi kuchana wala hawana ngoma zozote zinazotisha baadhi ya mastaa hao wamemjibu.

"Naskia Tanzania ma Rapper wameshika moto, yall have 24 hrs to go to the the studio and Record, na msiniletee amapiano, ingieni kwa kiwanja tupimane nguvu, you will respect the OG."

Miongoni mwa rappers ambap wameshindwa kujizuia na kuamua kumtolea povu, ni mwanadada Rosa Ree ambaye kwa sasa analea mtoto wake.

Rosa ameona isiwe tabu, haikufika hata saa 24, akajichukulia sheria mkononi kwa kudondosha verse kali ikiambatana na caption inayosema; "Naskia kuna mtu anajaribu kuvuka border. I’m the Best Rapper in AFRICA‼️"

Ikumbukwe kuwa, Rosa Ree alishawahi kuachia ngoma aliyomshirikisha Khaligraph iitwayo One Time remix.

Nimi maoni yako kwenye hili?

Chanzo: Mwanaspoti