Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rosa Ree afunguka sababu za kuficha ujauzito mpaka kujifungua

Cxeg Rosa Ree Rosa Ree afunguka sababu za kuficha ujauzito mpaka kujifungua

Fri, 9 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa rap Bongo, Rosa Ree akiwa kwenye #theswitch ametoa exclusive ya sababu zilizomfanya kuficha ujauzito wake na hata alipojifungua kuendelea kumficha mtoto mpaka alipoweka wazi mwaka huu kwenye siku ya mama duniani

Rosa Ree amesema kuwa alitaka kupitia hali ile ya ujauzito pamoja na kulea kivyake bila kuingiliwa na maoni ya dunia nzima

"Nilitaka kupitia ile 'experience' kivyangu. unajua social media (mitandao) inawaruhusu watu wote duniani kutoa maoni kuhusu maisha yako na mimi sikutaka kuingiliwa katika experience ambayo ningepitia na mwanangu, nilitaka nijifunze kuwa mama mwenyewe"

"Ilipofika siku ya mama duniani, niliona hii inanihusu ndio maana nikaamua kuweka wazi kuwa mimi ni mama," amesema Rosa Ree.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live