Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Ronaldo hutumia Tsh mil 47 kubadili oil ya gari

Ronaldos (11).jpeg Ronaldo hutumia Tsh mil 47 kubadili oil ya gari

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama utakuwa ni moja kati ya watu ambao wanandoto siku moja kuja kumiliki magari ya kifahari basi leo kwa uchache tunakufahamisha gharama za kubadilisha oil kwa magari baadhi ya kifahari.

Kupitia mtandao wa Bugatti Browad unaandika gharama za kubadili oil kwa magari hayo ni kuanzia Million 47,340,000 hadi Million 59,175,000 na kutofautia huku inategemeana na modeli ya Bugatti husika, na wauzaji wa magari haya pia wanashauri walau oil ibadilishwe mara moja kwa mwaka.

Mtandao wa J.D. Power unataja gharama za kubadili oil kwenye gari aina ya Lamborghini ni Kuanzia Laki 946,800 hadi Million 4,734,000 kwa kutegemeana na modeli ya Lamborghini husika, na inashauriwa kubadilishwa kwa kila baada ya Miles 9,000 ambayo ni sawa na Kilomita 14,484.

Mtandao wa Rolls-Royce Motor Car unataja gharama za kubadilisha oil kwenye gari hizo ni kuanzia Millioni 1,538,550 hadi Millioni 4,734,000 na hii pia inategemeana na modeli ya gari na mwaka husika, Kwa kawaida pia wameshauri kubadilishwa kwa oil wa gari hiyo kuanzia Kilomita 4,828 hadi 11,265 ambayo ni sawa na mara mbili hadi moja kwa mwaka.

Kwa upande wako unatumia muda gani kubadilisha oil ya gari yako? na huwa inakugharimu kiasi gani?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live