Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Romy amshauri Diamond aache kusaidia wasanii “wanakuponda, inatosha sasa”

MONDI NA ROMY Romy amshauri Diamond aache kusaidia wasanii “wanakuponda, inatosha sasa”

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaka yake Diamond Platnumz, Romy Jons, amemshauri binamu yake huyo kuacha kuwekeza kwa wasanii na badala yake ajikite kwenye Radio na Televisheni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Romy ameweka picha ya Diamond akiwa na Davido kisha kutiririka na bonge la ujumbe:

Barua ya wazi kwa mdogo wangu Nasibu Abdul ama Diamond Platnumz nakumbuka ulivyoanza kutoa nyimbo na wasanii tofauti na wa nchi tofauti soko lako hadi number zako zilikua kwa kasi sana kwenye mziki wako hadi kupelekea kua msanii bora afrika mashariki sio sababu wewe ndio ulikua unajua kuimba peke ako hapana!

Bali ulikubali kuwekeza muda,akili hadi pesa kwenye biashara yako hadi ikafika kipindi tukawa tunashangaa kolabo zako. Mara na Davido mara P Square mara Mr Flava na ndio watu waliokua wa moto kweli kweli kipindi hicho!!!

Ushauri wa wazi kwako!! Hata kama ni biashara ama kukuza vipaji vya mtaani nadhani sasa inatosha kwa nini usiwekeze nguvu, akili, pesa kwenye biashara yako ya Radio na Tv??

Wanasema “kikulacho kinguoni mwako” Walewale uliowafungulia njia ndio wapo nyuma yako kukukashifu, kukuponda hata kukukebehi!!

Tukiangalia top charts wasanii wote ni wale waliotoka kwako ama waliopo kwako hii ni wazi kwamba usingekua na wasanii number za mwanzo zote huenda zingekua za kwako kwa kipindi kirefu mno.

Ni kweli kila anaekua ana hitaji kutoka kwenye familia na kujitafutia ugali mwenyewe na kutengeneza familia yake sasa ni lazima kumponda ama kumkebehi mzazi wako??

Lil Wayne bado yupo na kina Drake na juzi wali-perform pamoja kwenye tamasha la Drake Usher Raymond bado yupo na Justin Bieber na anaendelea kunufaika na matunda yake. Sijajua huku kwetu ni ulimbukeni wa pesa nyingi za ghafla, tabia ama uelewa ni mdogo!!

Jaribu kuwekeza nguvu zako kwako mwenyewe tuone kwa sasa hivi huwenda ungekua na album moja na Chris Brown sasa hivi kuliko kuwekeza nguvu, muda kwa watu wasio na shukran!!!!

Naomba kuwasilisha! From your lovely brother

Wasanii walioondoka Wasafi mpaka sasa ni pamoja na Harmonize na Rayvanny hivyo kwa namna moja au nyingine mmoja kati ya hao au wote hauwenda ndio anaowazungumzia Romy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live