Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rommy Jones akiri kuhusu picha zake za utupu “nililewa, naomba radhi"

Rommy Jones Mkl Romy Jones

Wed, 3 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kaka wa Msanii Diamond Platnumz, RJ the DJ kwa mara ya kwanza kabisa amefunguka kuhusu sakata la picha za utupu wake kuvujishwa mitandaoni na mwanaharakati wa kimitandao, Mange Kimambi.

RJ amechukua fursa hiyo pia kuwaomba radhi mashabiki zake na wote waliokwazika na kitendo kile akisema kwamba hajui zilimfikiaje Mange ila anahisi ni fundi wa simu alizivujisha baada ya kumpelekea simu kuitengeneza.

"Zile picha zilizovujishwa na Mange ni za muda mrefu, nlirekodi nilikuwa nimelewa na sijui nani aliamua kuzivujisha. Kuna mtu alipigia simu miaka mitatu mine nyuma alinipigia ‘Nina picha zako za utupu, ili nisizisambaze nitumie milioni moja nizifute’, mimi nikashtuka nikamwambia sina pesa.

“Ile simu niliyokuwa natumia mwanzo iliharibila nikaipeleka kwa fundi ili aitengeneze, ni rafiki yangu yupo Mwenge, baada ya jamaa yule kunitumia picha zile nikaripoti Polisi Oysterbay nikapewa RB, akawa anatafutwa mara yuko Buguruni mara yupo Mbezi.

“Baadae akanitumia zile picha, ikabidi nimtumie mke wangu kumuuliza kama kwenye simu kuna hizo picha akakataa, nikamcheki fundi wangu kumuuliza kama ile simu ameiuza akasema hapana ila amei-flash, nikaenda kwake nikahakikisha kweli ame-flash hakuna picha yoyote," RJ the DJ alisema.

Rommy amewaomba radhi wote kuanzia familia yake ambayo ni mke wake, ndugu zake na pia mashabiki wa Wasafi kwa kitendo hicho.

"Nichukue fursa hii kuomba msamaha kwa Mungu, mke wangu, familia yangu pamoja na Mashabiki wangu wote haijalishi yalikuwa ya kweli au ya uongo," alisema Rommy.

Vile vile, msanii huyo alitumia fursa hiyo kufunguka siri za kudumu kwa ndoa yake ambayo imedumu muda mrefu ilhali mdogo wake, Diamond ameshindwa kudumisha ndoa hata miaka mitano mfululizo.

"Mara nyingi ndoa zinazodumu kwamuda mrefu ni zile ndoa ambazo nakwambia Diva mimi nataka kukuoa, kwa sababu mimi ndio mwanaume ninaeshikilia mahusiano yetu pia nashikilia familia yetu.

“Wewe ukiniambia tuone kwa sababu labda umeona shoga zako wanaolewa au ndugu zako wanasema huyu mwanaume mbona hakuoi umekaa naye muda mrefu, hapo utataka uolewe na mimi kwa sababu ya shinikizo.

“Mimi mke wangu hakuniambia tuoane bali mimi ndio nlimwambiatuoane kwa sababu mimi nlikuwa nipo tayari na ndio maana mpaka Sasa ndoa ipo," alisema DJ.

Usiku wa kuamkia jana, Rommy Joans ameshinda tuzo ya Dj Bora Afrika Mashariki katika tuzo za @aeau_awards.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live