Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma awajibu wanaomponda shwahiba wake Stamina

RomAa 225589785 Roma awajibu wanaomponda shwahiba wake Stamina

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii nguli wa HipHop Bongo, Roma Mkatoliki amewajibu baadhi ya mashabiki wanaoponda uandishi wa Stamina kuwa ni wa kitoto.

“Kaka angu Stamina baadhi ya raia wanamkaanga sana wakimsema Uandishi wake (Word Play) kuwa ni wa kitoto. Binafsi napenda anachokifanya coz mbona tuna Rappers wengi tu wana Uandishi wao sio tu ni wa kitoto but haueleweki.

“Yani hata ukimuuliza hapo ulitaka ku-Address nini hawezi kuwa na jibu coz haandiki uhalisia wowote yeye anachozingatia ni neno hili lina “Kina” fulani anatafuta lingine anasindikiza na neno linaloendana na kina hiko, hata kama sentesi haitaleta maana,” ameandika Roma.

Roma na Stamina wanaunda kundi la ‘Rostam’ ambao tayari limetoa hits kibao kama Kijiwe Nongwa, Huku ama vile, Kaka tuchati, kaolewa, parapanda, hujambo mwanangu, sifa na kibamia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live