Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma amlilia Rais Mkapa

57237de60e1789d99136f6da7d34bf8d.png Roma amlilia Rais Mkapa

Thu, 30 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MSANII wa Bongo Fleva, Ibrahim Musa ‘Roma’, amesema mchango wa Hayati Rais Benjamini Mkapa, kwenye tasinia hiyo hauwezi kusahaulika, kwani ulianza tangu akiwa madarakani mwaka 1995.

Amesema muziki wa Bongo Fleva ulianza kuwika kuanzia miaka ya 1990, hivyo ana amini Rais Mkapa alitengeneza miundombinu mizuri na ameacha alama kubwa iliyochangia muziki huo kuendelea kufanya vizuri, ikiwamo kuibua kizazi kipya cha wasanii wanaofanya vyema hadi kimataifa.

“Mchango wa Rais Mkapa hauepukiki kwenye maendeleo ya tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, kwani muziki wetu ulianza kuwika miaka ya 1990 kipindi ambacho kuliibuka wasanii wengi kuimba nyimbo nzuri na za kuelimisha na mwaka 1995 aliingia tena madarakani na uliendelea kufanya vizuri,” alisema Roma.

Mkapa aliyefariki wiki iliyopita, alizikwa jana kijijini kwao Lupaso, wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

Chanzo: habarileo.co.tz