Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma aikataa 2060 ya Madee

ROMA+PIC Roma aikataa 2060 ya Madee

Tue, 18 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By KELVIN KAGAMBO Rapa kutoka kundi la Rostam, Ibrahim Juma maarufu Roma Mkatoliki amemtambia mwanamuziki mkongwe wa Bongfleva Madee Seneda kwa kulinganisha wimbo wake wa 2030 dhidi ya wimbo mpya wa Madee 2060 akidai wimbo wake ni mkali zaidi.

Roma ametoa tambo hizo kupitia akaunti yake ya Twitter usiku wa kuamkia leo Agosti 18, huku akidai hazina mlengo wowote wa kuchochea bifu kati yao, bali ni kwa ajili ya kuchangamsha gemu tu.

“Leo Nimebishana Na @Madeeseneda Kwenye Simu Kwa Muda Kama Wa Masaa Matatu Kuhusu Hizi Nyimbo Mbili!! Ya Kwake Mpya inaitwa #2060 Na Ya Kwangu ile Inayoitwa #2030 Kwa Tulivyobishana Tungekuwa Karibu Tungepigana #MITAMA Wewe Shabiki Ndiyo Muamuzi Wa Mwisho Katika Hili!” ameandika hivyo Roma.

Mlingano wa nyimbo hizi mbili ukoje

Ukweli ni kwamba mfanano wa nyimbo hizi uko kwenye sehemu mbili tu, kwanza majina ya nyimbo, zote mbili zina majina ya miaka, mmoja mwaka 2030 mwingine mwaka 2060.

Lakini pili ni namna Roma ameufanya wimbo wake kama dedication kwa mtoto wake Ivan ambaye itakapofika mwaka 2030 atatimiza miaka 18, umri wa kupiga kura. Wakati Madee yeye katika wimbo wake amemshirikisha mwanae wa kike Chonge anayekaribia miaka miaka 6 ambaye kwa pamoja wameimba kiitikio cha wimbo huo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz