Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma: Wasanii msidharau kazi za wasanii wenzenu

Roma Mtoto Roma Mkatoliki

Tue, 14 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa nguli wa Bongo, Ibrahim Mussa Mashana maarufu kama Roma Mkatoliki ameonyesha kukerwa na tabia za baadhi ya wasanii kudharau kazi za wengine.

Roma ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani, ametumia ukurasa wake wa Twitter kuelezea akisema; “Ewe msanii kama unataka kutoa wimbo wako wewe toa tu na upromote kimpango wako pasi ku-underrate efforts za wasanii wenzako.

"Hii tabia unatoa wimbo then ukihojiwa unasema, ‘ujue game hapa katikati ilikuwa kama imelala hivi so nimeona nije kuichangamsha.’

"Sikia mwanangu, game haijawahi kulala hata siku moja. Madogo wanapiga kazi na wanakichafua haswaa kama huwaoni sisi tunawaona. Unamskia msanii anasema, ‘unajua hip hop ililala saaana hapa katikati, nimekuja sasa kuiamsha.’

"Weee bwana hebu usitukwaze, tena hapo kwenye Hip-Hop ndio usipaguse kabisaaaaa tutagombana sana. Hip-hop haijawahi na haiwezi kulala….milele yote!!

"Nimeandika kwa hisia kali sana na uchungu mithili ya #msimbe aliyenyimwa urithi,” amesema Roma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live