Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma Mkatoliki siyo mwana harakati - Wakazi

Wakazi Romaaaa.jpeg Roma Mkatoliki na Wakazi.

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vita ya maneno na spana bado zinaendelea huko mtandao wa X baada ya rapa Wakazi kumchana Roma Mkatoliki akimwambia sio mwanaharakati kama anavyojinasibu.

Wakazi amefunguka hilo baada ya kuandika kuwa; “Roma labda uwadanganye wapwa ila sio sisi watu wazima wenzako. Sio mwanaharakati kiivyo kama unavyojinasibu”

“Wewe ni Msanii wa kusema vitu for shock value, upate reaction kisha Media zikupige na kukupa shows. Mzee wa Hit Song wakati hit zenyewe wanazo kina Darassa, AY, Chid Beenz,” amesema Wakazi.

Vita yao hiyo ya maneno inaenda kumaliza mwaka sasa na ilianzia mtandao wa X kwa kila mmoja kushea maoni yao kuhusu muziki na uwezo wa binafsi kama wasanii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live