Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma Mkatoliki awafunda wasanii wenzake

8d737b926e3ec193884c935d538bdb9e.jpeg Roma Mkatoliki awafunda wasanii wenzake

Thu, 10 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANAMUZIKI wa kizazi kipya, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’ amewataka wasanii wenzake wanaponadi wagombea wao kupitia nyimbo zao waache kuzungumzia mabaya ya chama kingine ili kuepusha kuwagawa mashabiki.

Akizungumzia mtazamo wake huo alisema msanii anatoa wimbo wa kampeni kwa ajili ya kusifu, au kueleza maendeleo ya chama fulani ni kitu kizuri sana, lakini waepuke kuzungumza mabaya ya chama kingine au kiongozi wa chama kingine.

Anasema unapofanya hivyo chama unachokipigia kampeni kikipata kura milioni 8 na hicho chama kingine kikipata kura milioni 6, hivyo kama utakuwa umetoa kauli mbaya utakuwa umewakwaza hao watu milioni sita.

“Lakini niwashauri kitu kimoja kama itawapendeza, kwenye nyimbo hizo mnazotoa epukeni tungo zinazowazungumzia wapinzani kwa vyama hivyo mnavyovinadi”

Roma alipata umaarufu mkubwa sana, baada ya kutoa nyimbo ambazo zilikuwa zikizungumzia masuala mbalimbali ya Kiserikali.

Chanzo: habarileo.co.tz