Menu ›
Burudani
Mon, 27 May 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Rapa Roddy Ricch amefikiana makubaliano na Ex wake juu ya malezi ya mtoto wao mwenye umri wa miaka mitatu. Roddy amepatiwa haki ya kumuona mtoto wake angalau mara mbili kwa wiki (Jumanne na Alhamis)
Nyongeza ya hilo, Roddy Ricch ametakiwa kulipa kiasi cha ($8,000) takribani TSh. Milioni 20 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ikiwemo gharama kama mahitaji ya shule, gharama za matibabu na matumizi mengine.
Aidha pia amekubali kulipa gharama za kuendesha kesi ($37,500) zaidi ya TSh. Milioni 97 ambazo Ex wake (Alexandra Kiser) alizitumia kufungua shauri hilo.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live