Mhandisi wa programu wa Tesla kutoka nchini Marekani mbaye jina lake halijawekwa wazi amepata majeraha mkononi na mgongoni baada ya kushambuliwa na ‘roboti’ kwenye kiwanda cha kutengeneza magari ya umeme cha kampuni hiyo iliyopo Texas.
Inaelezwa kuwa ‘Roboti’ hiyo iliyotengenezwa kwa ajili ya kusogeza sehemu za gari za aluminum, ilimkaba mwanaume huyo na kuzamisha makucha yake ya chuma mgongoni na kwenye mkononi wa kushoto, wakati akiweka ‘programu’ kwa robot mbili za Tesla zilizokuwa hazifanyi kazi.
Tukio hilo lilipelekea mwanaume huyo kupata majeraha na kutokwa damu nyingi, na kusababisha kuzuka taharuki kwa wafanyakazi kuhusu usalama wao na mahusiano kati ya binadamu na ‘roboti’ kwenye viwanda vya Tesla.