Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Risa Hirako: Nina miaka 51

Hirako .jpeg Risa Hirako

Sun, 4 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamitindo wa nchini Japan, Risa Hirako awaacha mashabiki midomo wazi na kuibua minong'ono baada ya kueleza kuwa umri wake halisi ni miaka 51 wakati asilimia kubwa ya watu walikuwa wanadhani umri wake hauzidi miaka 25.

Kufuatia kutaja umri wake halisi watu wamemuomba pia aeleze siri ya muonekano wake wa kuvutia ikiwemo ngozi.

Risa ameeleza siri ya kuendelea kuonekana binti mbichi ni kuishi mtindo wa maisha yenye afya, amesema yeye anapendelea kula vyakula asilia na vipodozi asilia, hapendelei kula vyakula vya viwandani wala hapendi kuiumiza ngozi yake kwa kutumia vipodozi au bidhaa zenye sumu.

Lisa pia anapokuwa nje ya nyumbani hupendelea kuvaa kofia na mavazi yanayoikinga ngozi yake dhidi ya miale ya jua kali ambayo ina athari mbaya katika ngozi.

Hata kabla mrembo huyo hajataja umri wake halisi, kwa muda mrefu amekuwa akionekana anapenda kula zaidi vyakula asilia yakiwemo matunda kama parachichi na mengineyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live