Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna kurudi kwa kishindo kwenye muziki

Rihanna Twitter Rihanna

Sun, 22 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani, Rihanna anadaiwa kuwa yupo kwenye mipango ya kurejea kwenye muziki kwa kishindo ambapo anatarajia kufanya ziara kubwa ya muziki mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vinaeleza kuwa kurejea kwa mwanamuziki huyo ni kutokana na kusaini ‘dili’ nono lenye thamani ya ($32 million) ambazo ni zaidi ya Bilion 80 za kitanzania na ‘kampuni’ ya Live Nation.

Ujio huo unatajwa pia utasindikizwa na ‘album’ zake mbili ambazo ataziachia kuelekea ziara hiyo.

Ikumbukwe kuwa msanii huyo mwenye watoto wawili sasa, alipumzika kuimba kwa muda kwasababu zake binafsi, huku wimbo wake wa mwisho kutoa ni ‘lift me Up’ alio uachia miezi 11 iliyopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live