Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna hana mpango wa kufanya ziara

Rihanna.jfif Rihanna hana mpango wa kufanya ziara

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzuka tetesi kuhusiana na msanii #Rihanna kuwa anapanga kufanya Tour kubwa mwaka 2024, kwa mujibu wa #Billboard imefichua taarifa hizo ni za uongo.

Siku ya Jumapili baadhi ya vyombo vya habari nchini #Marekani viliripoti kuwa #Rihanna anatarajia kufanya ziara kubwa Dunia ambapo ameingia mkataba wa Dola 39 milioni na Live Nation.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha msanii huyo kimeeleza kuwa Rihanna bado hajathibitisha ziara yoyote kwa mwaka 2024.

Aidha, Billboard inaripoti kuwa Live Nation haijafika kwenye kumbi zozote kufanya booking kwa ajili ya ziara yoyote.

Ikumbukwe ziara ya mwisho aliyoifanya ni mwaka 2016 ya ‘Anti World Tour’ ambayo aliingiza zaidi ya dola 100 milioni kwa mauzo duniani kote huku sehemu ya mwisho ya zaira hiyo ikiwa ni ‘Abu Dhabi’ Novemba 27, 2016 na mpaka sasa hajafanya tena ziara yoyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live