Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna autema Uongozi Kampuni ya Fenty

Rihaanna Resign Rihanna

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rihanna ameachia ngazi kama CEO wa Kampuni yake ya Savage X Fenty, umeripoti mtandao wa Vogue.

Jarida hilo limeeleza kwamba, limefanya mazungumzo na Riri ambaye amesema, anaona fahari kwa kile ambacho amekifanikisha na chapa yake.

“Imekuwa ni nzuri kuona matarajio yetu kwa Savage X Fenty yameleta mchango chanya kwenye kiwanda katika kipindi cha miaka 5.

Huu ni mwanzo tu kwetu, tutaendelea kupanuka kwa namna kwamba siku zote tunaungana na wateja wetu.” amekaririwa Riri.

Kwa namna ya kipekee ametumia muda huo pia kumtambulisha CEO mpya ambaye anaamini ataisukuma Kampuni mbele zaidi, “Nina furaha na shahuku kumtangaza Bi. Hillary Super kama CEO wetu mpya.

Ni kiongozi mwenye nguvu na amejikita kwenye kuipeleka biashara kwenye hadhi ya juu zaidi.” alimaliza Rihanna.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live