Rihanna, ambaye alitumbuiza kwenye halftime la Super Bowl 2023, ametoa maoni yake kuhusu Kendrick Lamar ambaye atachukua nafasi hiyo mwakani.
Katika mahojiano na Kevin Frazier wa Entertainment Tonight, Rihanna alifunguka, “Ni kama alama ya thamani kwenye kidole, inapaswa kuwa hivyo!”
Rihanna alimsifu Lamar kama msanii bora, akisisitiza kwamba ana uwezo wa kufanya vizuri na kwamba amekuwa na mwaka mzuri sana, na ameleta watu pamoja. Aliongeza kwamba anasubiri kwa hamu onyesho lake.
Kwenye Super Bowl 2023, Rihanna aliweka wazi kwa mara ya kwanza kuwa na ujauzito wa mtoto wa pili na A$AP Rocky na onyesho lake liliweka rekodi ya watazamaji milioni 121, japo Usher alivunja rekodi hiyo mwaka huu kwa watazamaji milioni 123.