Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna anarudi kwenye Super Bowl 2023 kwa kishindo

RihannaFENTY Rihanna

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa muziki Bad Gal Riri, "Rihanna" anarudi kwenye Super Bowl 2023 kwa kishindo, hii ni baada ya mwaka 2019 kuipiga chini ofa ya kutumbuiza kwenye fainali hizo.

NFL imethibitisha rasmi kuwa Rihanna ndiye msanii kinara atakayeipamba “Half Time” show ya fainali za Super Bowl 2023 ambayo inatarajiwa kufanyika Februari 12.

Fahamu, burudani inayotolewa kwenye fainali za Super Bowl (wakati wa mapumziko) ni miongoni mwa burudani maarufu zaidi zenye watazamaji wengi duniani kote.

Msimu uliopita kwenye fainali hizo, burudani ilitolewa na wakali Dr. Dre, Snoop Dogg, Eminem, Mary J. Blige, Kendrick Lamar, 50 Cent na Anderson Paak.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live