Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna ampa Tuzo Jay Z

Jay Z Rihanna .jpeg Rihanna ampa Tuzo Jay Z

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkongwe wa Rap kutoka Marekani, Jay-Z ameshinda tuzo ya 'Director Bora' katika tuzo za ‘Emmy Primetime Creative Arts 2023 ikiwa ni tuzo yake ya tatu ya Emmy yote ni baada ya kushiriki kama muongozaji wa show ya Super Bowl ambayo Rihanna alitumbuiza Februari 2023.

Shoo hiyo pia ilishinda ubora wa aina maalum, miongozo bora ya muziki na ubunifu wa uzalishaji bora. Pia iliteuliwa kwenye kipengele cha ubora wa mchanganyiko wa sauti.

‘Rihanna ni kipaji cha kizazi, mwanamke mwenye mwanzo mnyeyekevu ambaye amevuka matarajio kila kukicha. Mtu aliyezaliwa kwenye kisiwa kidogo cha Barbados ambaye amekuwa mmoja wa wasanii maarufu zaidi. Amejitengeneza mwenyewe kwenye biashara na burudani’ alisema Jay Z baada ya Rihanna kutangazwa kutumbuiza ‘Super Bowl LVII’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live