Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rihanna: Mtoto wangu amerithi komwe langu

Rihanna Asap Rocky Rihanna: Mtoto wangu amerithi komwe langu

Wed, 20 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Staa wa muziki duniani Rihanna amefunguka experience ya kuwa mama wa familia na rapa ASAP Rocky kuwa baba wa watoto wake wawili wa kiume ambapo ameshangazwa na mtoto wake mmoja Raz kufanana naye Komwe.

Rihanna anasema mpenzi wake na mzazi mwenziye ASAP Rocky ni baba wa tofauti, mvumilivu, kiongozi, mwenye upendo na watoto wake wanavutiwa naye.

“Nilimpenda tofauti kama baba. Ni kiongozi mkubwa, mvumilivu, mwenye upendo na watoto wangu wanavutiwa naye. Wanampenda baba yao kwa njia tofauti na ninapenda kuwaona”.

“Nilikuwa natamani kuwa na watoto siku 1, kuwa sehemu ya familia, kizazi na kulea watoto zaidi ya tulivyolelewa sisi. Kitu pekee nilichofikiria labda ni paji la uso kwenye RZA ‘Komwe’ lakini Rizza Riot hana komwe”. amesema Rihanna

Ungependa mtoto wako arithi nini kutoka kwako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live