Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rick Ross mbioni kujenga nyumba chini ya ardhi

Rick Ross Bil ‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Rick Ross

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Rick Ross ameweka wazi kuwa anampango wa kujenga nyumba chini ya Ardhi ambayo itakuwa na chumba cha kulala, gereji na mashine inayotengeneza maji kutoka angani.

Kupitia video inayosambaa mitandaoni inamuonesha Rick akieleza kuwa atajenga chumba hicho kwa lengo la kujiandaa na maisha yake ya siku ya mwisho.

Mbali na kutaka kujenga mjengo huo Rick pia anamiliki ndege binafsi (private jet), eneo la hekari 2.3 kwa ajili ya mapumziko lililopo Florida, na Jumba la kifahari la ‘Star Island Waterfront'.

Ikumbukwe pia baadhi ya matajiri dunia kama vile Elon Musk na Mark Zuckerberg tayari wamejenga nyumba za aina hiyo chini ya ardhi,zijulikanazo kama ‘Bunkers’.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live