Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rick Ross kumlipa Mil. 287.5 mfanyakazi wa ndege yake binafsi

Rick Ross Kumlipa Mil. 287.5 Mfanyakazi Wa Ndege Yake Binafsi Rick Ross kumlipa Mil. 287.5 mfanyakazi wa ndege yake binafsi

Wed, 15 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa na mfanyabiashara kutoka Marekani Rick Ross ametangaza kuajiri mhudumu wa Ndege atakayefanya kazi kwenye ndege yake ya kibinafsi, ambapo atamlipa hadi kiasi cha dola 115,000 sawa na sh Mil. 287,500,000.

Tajiri huyo mmiliki wa ndege za Bel Air alitangaza hili katika video moja ambayo imeenezwa mitandaoni ambapo amesema kwamba anatafuta mhudumu mwenye ucheshi na umahiri wa juu katika kufanya kazi yake.

“Niaje, huyu ni bosi mkubwa kwenye kaya, hapa nyuma yangu ni ndege yangu ya Bel Air. Bosi Rick Ross anatafuta mhudumu wake wa kibinafsi katika ndege yake ya kibinafsi. Mshahara ni kati ya dola elfu 85 hadi dola elfu 115 kwa mwaka. Ni lazima uwe na uzoefu, uwe mchangamvu na uwe vizuri katika kumhudumia Ross…” msanii huyo alisema.

Ross alisema kwamba kwa kawaida kuzunguka katika maeneo mbalimbali kote ulimwenguni kumekuwa moja kati ya biashara zake nyingi na hivyo kuona haja ya kupata mhudumu wa kibinafsi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live